GIDAMIS SHAHANGA NDIYE MWANARIADHA MTANZANIA WA KWANZA KUWEKWA KWENYE STAMP YA TANZANIA YA MWAKA 1980

June 29, 2013

 GIDAMIS SHAHANGA ni mwanariadha maarufu sana wa miaka ya 70 naa... hadi 1990 aliyeliletea Taifa letu la Tanzania heshima na rekodi isiyofutika katika rekodi sahihi za riadha nchini Tanzania na kote duniani.

Gidamis ndiye mwanariadha wa kwanza hadi sasa ambaye picha yake iliwekwa katika STAMP (ya barua) ya Tanzania mnamo mwaka 1980 wakati wa utawala wa Mhasisi wa Taifa la Tanzania Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Gidamis Shahanga ni mwanariadha mstaafu aliyekuwa amejikita katika  mbio ndefu za mita 10,000 na mbio za Marathon. Shahanga alizaliwa Septemba 4, 1957 kaskazini mwa Tanzania yani Katesh Wilayani Hanang Manyara.

 Kutoka kushoto (25) ni Zacharia Barie (Mtanzania) na katikati (26) ni GIDAMIS SHAHANGA wakimuonyesha umahiri mkenya (23) katika mbio zilizofanyika San Juan Porto Rico miaka ya 1980.

 Ni vyema serikali na wadau wa michezo nchini kuwaenzi wachezaji wa zamani walioliletea Taifa letu heshima katika michezo mbali mbali hapa nchini kama Gidamis Shahanga. Kwa pamoja Site hii ya Asili Yetu Tanzania inampongeza sana bwana Gidamis Shahanga kwa kuonyesha ushujaa wake katika mchezo wa riadha hapa nchini miaka ya 70.

 HAYA NI BAADHI YA MAFANIKIO YAKE YA KIMATAIFA
 
 
 
Source: Victormachota.

Comments

Popular

GIDABUDAY KUHAMASISHA UJENZI WA KIJIJI CHA MICHEZO TANZANIA LENYE JINA YA MWANARIADHA MKONGWE BW.JOHN STEPHEN AKHWARI

Rio Olympics: Brazil win men's volleyball gold, GB's Joyce takes boxing silver – as it happened

Olympics 2016: Usain Bolt completes sprint double, Jade Jones retains taekwondo title

Rio Olympics: Swimmer Lochte apologises for 'robbery' saga