PHAUSTIN BAHA SULLE: MWANARIADHA ALIYEKATAA KUPOKEA ZAWADI BILA BENDERA YA NCHI YAKE KUPEPEA MBELE YAKE AKIWA VERACRUZ MEXICO

Mwanzo wa mashindano ya dunia mjini Veracruz Mexico, Tanzania ilipata medali ya Fedha kupitia mwanariadha Phaustin Baha Sulle

Ilikuwa katika mbio za Lisbon Half Marathon 2000 ambapo wanariadha kutoka Kenya, Ethiopia, Moroco, Tanzania, Ulaya, Marekani na Asia walipokutana nchini Ureno kushiriki mashindano hayo makubwa duniani.
Phaustin Sulle nyuma ya Paul Tergat

Paul Tergat wa Kenya aliyekuwa akishikilia rekodi ya dunia ya nusu marathon kwa wakati huo alikuwepo katika mstari wa kuanzia mbio. 

Wanariadha wote walikuwa wakimtazama Tergat na wakenya wenzake, hawakujua kuna kijana chipukizi kutoka Babati Tanzania ambaye hakujali nani yupo, yeye alisubiri kwa hamu mbio zianze. Muda mfupi baadaye Paul Tergat alijikuta akitolewa jasho na Phaustin Baha Sulle kuanzia kilomita ya kwanza hadi ya kumi.

Ndipo sasa Tergat alipotumia uzoefu wake kumdhibiti Sulle hatimaye Tergat alishinda mbio hizo kwa umbali mdogo sana kati yake na Phaustin Baha Sulle. Tergat alikimbia dakika 59:34 na Sulle nyuma yake kwa 59:36. Rekodi hiyo ilimfanya Sulle kuwa mtanzania wa kwanza kukimbia chini ya saa moja na pia alivunja rekodi ya vijana ya dunia papo hapo.

Miezi sita baadaye Tergat na Sulle walikutana mjini Veracruz Mexico katika mashindano ya dunia ya nusu marathon ambapo Tergat kwa mara nyingine alitokwa jasho kwa kumshinda Sulle kwa sekunde moja, ambapo Sulle aliiletea Tanzania medali ya Fedha.  “Nilikataa kupokea zawadi maana bendera ya Tanzania haikuwepo; wamexico waliheshimu msimamo wangu wakasubiri bendera ilipoletwa ndipo tukakabidhiwa zawadi zetu” alisema Sulle.

Je watanzania wanafahamu kwamba zaidi ya Bayi na Nyambui kuna walioweka historia nzuri zaidi?. ‘Imezoeleka kwamba kumbukumbu zinazoandikwa kila mara itamtaja Bayi na Nyambui pekee wakati kuna wengine ambao walifanya vyema na wakaamua kukaa zao kimya.  

Kukaa kando ni uzalendo zaidi kuliko hao wanaotajwa kila siku ambao wamekuwa ving’anganizi katika uongozi wa vyama vya michezo ili kujinufaisha wao wenyewe’.

Comments

Popular

GIDABUDAY KUHAMASISHA UJENZI WA KIJIJI CHA MICHEZO TANZANIA LENYE JINA YA MWANARIADHA MKONGWE BW.JOHN STEPHEN AKHWARI

Rio Olympics: Brazil win men's volleyball gold, GB's Joyce takes boxing silver – as it happened

Olympics 2016: Usain Bolt completes sprint double, Jade Jones retains taekwondo title

Rio Olympics: Swimmer Lochte apologises for 'robbery' saga