UHURU MARATHON: Sintofahamu yaibuka baina ya jamii ya wanariadha kuhusiana na hali ya mkenya anayedaiwa kuugua ghafla baada ya mbio za jana

Tetesi za kuzidiwa ama hata kufariki kwa mwanariadha wa Kenya zinazidi kuwa tata baada ya simu za wahusika wa RT na wakala aliyewaleta wakenya hao kutopokelewa ama kuwa zimezimwa.

Hata hivyo kwa kutumia simu nyingine mwanahabari moja ameweza kuongea na katibu wa RT Suleiman Nyambui na kugundua kuwepo na hali ya wasiwasi katika majibu yake.

Nyambui alinukuliwa akisema "Hadi jana baada ya mbio sijasikia chochote ila kuna wanariadha wawili mmoja akiwa mkenya walioonyesha kujisikia vibaya, nikawanunulia ugali wa dona na wakaondoka hivyo baada ya hapo sijui kilichoendelea".

Aliendelea kusema "Nitakwenda Mwananyamala Hospital alafu baadaye tuwasiliane". Hali iliyoshangaza ni kwamba alijuaje tatizo lipo Mwananyamala Hospital?. 


Katika maongezi hayo yaliyorekodiwa Nyambui pia alionyesha hali ya kujihami (Diffence) kwa kudai "Hata kikitokea kitu sisi hatutahusika maana waandaaji siyo sisi".

Awali ilithibitika kwamba hapakuwa na maji njia nzima wakati wa mashindano, kitu ambacho ni hatari na ni kinyume na maadili ya marathon. 

Tetesi zaidi ambazo zinavuma kutoka pembe tofauti ya watu zinadai kuna jambo baya linaweza kuwa limetokea.

Blogu moja maarufu nchini alfajiri ya leo ilitoa habari za kifo cha mwanariadha wa Kenya kutokana na kuishiwa maji mwilini, katika hali isiyo ya kawaida habari hiyo ilikuwa blocked masaa machache baadaye.

Wanariadha na watanzania wanasubiri kauli kutoka kwa RT na waandaaji wa Uhuru Marathon, ibainika kwamba kuna jaribio lolote la kuficha ukweli nchi ya Kenya watatulaumu sisi watanzania. 


'Lakini tusubiri tamko tukiendelea kuomba kwamba hakuna baya lililotokea'.

TUNAWASIHI RT WATOE TAMKO LA KUELEWEKA!

Comments

Popular

GIDABUDAY KUHAMASISHA UJENZI WA KIJIJI CHA MICHEZO TANZANIA LENYE JINA YA MWANARIADHA MKONGWE BW.JOHN STEPHEN AKHWARI

Rio Olympics: Brazil win men's volleyball gold, GB's Joyce takes boxing silver – as it happened

Olympics 2016: Usain Bolt completes sprint double, Jade Jones retains taekwondo title

Rio Olympics: Swimmer Lochte apologises for 'robbery' saga