Sugu atikisa Uwanja wa Sokoine

Sugu sugu sugu… hivyo ndiyo mashabiki wa Mbeya City walivyoimba kwa muda mrefu baada ya mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ kuingia uwanjani juzi kushuhudia mechi ya Ligi Kuu kati ya Mbeya City na Coastal Union.

Ilikuwa katika dakika ya 38 ya mchezo huo, wakati Sugu alipoingia uwanjani na baada ya kushuka tu kwenye gari lake, uwanja mzima ulizizima kwa kelele za mashabiki kumshangilia kwa nguvu zote  wakisema “Sugu sugu sugu”, huku wakimtaka aende kukaa kwenye eneo walilokuwapo. Sugu alilikubali wito huo na kwenda kukaa eneo la mashabiki hao.
Mmoja wa viongozi waliokuwa kwenye jukwaa kuu alishuka ghafla kwa lengo la kumkaribisha Sugu meza kuu, lakini Sugu hakwenda na badala yae alinyosha njia kwenda kukaa kwa mashabiki huku akishangiliwa kwa nguvu.
Akizungumza na gazeti hili, baada ya kumalizika kwa mechi hiyo, Sugu alisema hakuwa na sababu yoyote ya kukaa jukwaa kuu kwani uhondo wa mchezo ni pale unapokuwa na vijana aliowaita wenye ‘mizuka’.
“Utaendaje kukaa jukwaa kuu wakati masela wenye mizuka wapo na raha. Michezo ni mizuka ya mashabiki hivyo ni lazima nikajumuike nao kuishangilia timu yetu,” alisema Sugu.
Kabla ya mechi hiyo kuanza, mamia ya mashabiki wa Mbeya City walifanya maandamano yasiyokuwa rasmi na kufunga barabara kuu ya Dar es Salaam - Zambia wakati wakielekea kushuhudia mechi hiyo kwenye Uwanja wa Sokoine.
Mashabiki hao walikusanyika kwenye kituo cha daladala cha  Kabwe kuanzia saa 7:00 mchana, walianza msafara saa 9:05 alasiri wakiwa kwenye mabasi matano wengine wakitembea wa miguu. Walitumia takribani saa moja kufika uwanjani.

CHANZO: Mwananchi

Comments

Popular

GIDABUDAY KUHAMASISHA UJENZI WA KIJIJI CHA MICHEZO TANZANIA LENYE JINA YA MWANARIADHA MKONGWE BW.JOHN STEPHEN AKHWARI

Rio Olympics: Brazil win men's volleyball gold, GB's Joyce takes boxing silver – as it happened

Olympics 2016: Usain Bolt completes sprint double, Jade Jones retains taekwondo title

Rio Olympics: Swimmer Lochte apologises for 'robbery' saga